WUWE

 

 

 

 

  TAASISI YA UELIMISHAJI WANAWAKE YA USAMBARA MAGHARIBI******KUMUELIMISHA MWANAMKE NI KUIELIMISHA JAMII NZIMA!

Sep 26, 2008

SIKU YA KUADHIMISHA JIKO LA UKOMBOZI

Mnamo tarehe 12 Juni 2004, Taasisi ya WUWE ilifanya sherehe za maonesho ya teknolojia mbalimbali ambazo wanashughulika nazo. Teknolojia hizo ni pamoja na majiko sanifu ya kuni na mkaa, oveni za kuchomea nyama, oveni a kuokea mikate, umeme wa jua na majiko ya vikapu yasiyotumia nishati ya moto (majiko bubu) na makaushio bora ya mboga na matunda.


Katika siku hii, viongozi mbali mbali wa serikali na vyama vya siasa walialikwa, pamoja na wananchi wengine kutoka Lushoto mjini na vijiji mbali mbali vya wilaya ya Lushoto. Mgeni rasmi alikuwa ni Bw Mtanga, afisa mipango wa wakati huo wa wilaya ya Lushoto. Ilikuwa ni siku ya kukumbukwa sana, kwani maonesho ya teknolojia za nishati yaliongeza hamasa kwa wananchi kutaka kutumia teknolojia ambazo zilikuwa katika maonesho kwa siku hiyo.
Maandamano, kutoka ofisi za WUWE kwenda ukumbi wa CCM Lushoto




Sheikh Abdi Majaja akisoma utaratibu wa ufunguzi wa sherehe.






Akina mama wakiimba kwaya




Washiriki wakifuatilia hotuba

Akina mama wakifuatilia sherehe


Afisa kutoka TaTEDO akitoa ufafanuzi jinsi oveni ya kuchomea nyama inavyofanya kazi


Wageni wakiangalia teknolojia za umeme wa jua


Wageni waalikwa wakiangalia bidhaa zilizokaushwa kwa kaushio bora


Wageni wakipata maelezo jinsi oveni ya kuokea mikate inavyofanya kazi


Baadhi ya majiko sanifu ya kuni na mkaa yaliyokuwa katika maonesho

Oct 29, 2007

JIKO LA UKOMBOZI

Jiko hili ni maarufu sana maeneo mengi ya mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Pwani, Morogoro na Kagera. Ni jiko la kisasa la kuni, linalotengenezwa kwa kutumia udongo wa kichuguu, samadi mbichi, majivu, maji na majani yanayoteleza. Mchanganyiko huu hufanya jiko hili kutunza joto na hivyo kufupisha muda wa kupika vyakula. Limetengenezwa maalum kuzuia upotevu wa joto na halitoi moshi mwingi kama yalivyo majiko mengine ya asili.
Linatengenezwa kulingana na mahitaji ya mteja. Taasisi ya WUWE imekuwa ikitoa mafunzo kwa mafundi mbali mbali namna ya kutengeneza jiko hili katika mikoa tajwa hapo juu. Mafunzo haya yameonyesha mafanikio, kwani upokeaji wake umekuwa wa kuridhisha.

Picha: Jiko la Ukombozi kabla halijaanza kutumika.

Aug 6, 2007

UKAUSHAJI WA MBOGA NA MATUNDA

Tangu mwaka 2004, taasisi ya hii imekuwa ikijishughulisha na ukaushaji wa mboga na matunda kwa kutumia kaushio bora la mionzi ya jua. Kaushio hili, limejengwa mfano wa banda kwa kutumia mbao na karatasi ngumu ya nailoni aina ya 'Visquin', ambayo huhifadhi joto linaloingia katika kaushio hilo. Lina matundu maalumu ya kuingizia na kutolea hewa.


Kwa ndani, kaushio hili lina trei maalumu ambazo zimetengenezwa kwa mbao na nyuzi ngumu za nailoni zisizoathiriwa na jua.

Kaushio hili linaweza kukausha mboga, nyama na matunda kwa muda mfupi, iwapo kuna jua la kutosha.

Kaushio la Jua, linavyoonekana kwa nje

Maandalizi ya Matunda (hayo matunda katika beseni ni matufaa)kwa ajili ya ukaushaji. Kwanza yanamenywa, yanaoshwa na kisha hukatwa katika vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kukauka





Matunda yaliandaliwa yakiwekwa katika trei

Matunda yaliyokauka, huondolewa katika kaushio na kuhifadhiwa mahali pakavu kabla ya kufungashwa.

Apr 7, 2007

MAJIKO SANIFU YA KISASA (UKOMBOZI)

Kwa muda wa miaka minane ambayo WUWE imekuwa ikifanya kazi yake, imekuwa ikitengeneza majiko sanifu ya kuni yanayofahamika sana kwa jina la "Ukombozi". Jiko hili la ukombozi, limepewa jina hilo kutokana na kumkomboa mwanamke katika kazi ya kutafuta kuni mara kwa mara. Jiko hili linatumia kuni chache sana, ukilinganisha na jiko la majifya matatu, ambalo ni maarufu kwa maeneo mengi ya Tanzania.


Dr Mary wa kituo cha Afya Ruanda, katika wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya anasema "Tangu nimejengewa jiko la Ukombozi, limenipunguzia sana matumizi ya kuni". Anaeleza zaidi kwa kusema, "Kabla ya kuwa na jiko hili, nilikuwa natumia kuni za shilingi 2000 kwa wiki, lakini baada ya kujengewa jiko hili na Mama Mmbaga mwaka 2001, kwa sasa natumia kuni zisizogharimu zaidi ya shilingi 1000 kwa wiki" Maelezo kama haya pia yanatolewa na Mama Fatma Mkangama wa kijiji cha Umwe Kati, wilayani Rufiji, katika mkoa wa Pwani. Huyu naye ni kati ya watu waliojengewa majiko haya maarufu ya Ukombozi.





Kimsingi, jiko la ukombozi hutengenezwa kwa teknolojia rahisi, lakini iliyo makini sana. Jiko hili hutengenezwa kwa kutumia mchanganyiko maalum wa udongo wa kichuguu, samadi mbichi, maji na majani maalumu yanayoteleza, kwa kutumia vipimo maalum. Bidhaa hizi kuchanganywa na kufinyangwa pamoja na kufanya mchangayiko mgumu. Mseto huu ndio hutumika kujenga jiko hili. Baada ya jiko kujengwa, huwa tayari kwa matumizi baada ya kukauka kwa wiki mbili.


WUWE inaendelea kusambaza teknolojia hii kwa kasi katika mikoa mbali mbali. Mikoa ambayo imeshafaidi teknolojia hii ni Morogoro, Pwani, Tanga, Mbeya, Kagera, Kilimanjaro, Manyara na Arusha. Malengo ya taasisi hii ni kusambaza teknolojia hii kwa Tanzania nzima.














Pichani: Mafundi wa WUWE wakijenga jiko la Ukombozi

JINA LETU: WUWE
MAHALI TULIPO: LUSHOTO, TANGA, Tanzania
KUHUSU WUWE:
ZAIDI

YALIYOMO

MASKANI
WANACHAMA WETU
WASILIANA NASI

WASHIRIKA WETU

WANACHAMA WETU
TaTEDO
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO
CAMARTEC

WORLD DAY OF PRAYER
GDS

WUWE

Karibu katika tovuti hii ya WUWE. Hapa tutakuwa tunaweka mada mbali mbali ambazo zinahusiana na kazi zetu, ambazo lengo lake ni kuwasaidia wanawake kwa namna mbalimbali, hasa katika masuala ya elimu na ujasiriamali. Tunaamini kuwa kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima, hivyo tukisaidiana kutoa elimu tunaamini tutafanikiwa.

HIFADHI

WUWE





 

MSANIFU: MWALYOYO


©WEST USAMBARA WOMEN EDUCATION (WUWE) 2007. All rights reserved.